Berlin,Ujerumani.
Javier "Chicharito" Hernandez ameondoa gundu la kucheza michezo mitano ya Bundesliga bila kufunga goli baada ya jana ijumaa usiku kufunga goli la 15 na kisha kutengeneza jingine katika ushindi wa Bayer Leverkusen wa magoli 3-0 dhidi ya Vfl Wolfsburg huko BayArena.
Akitokea benchi Chicharito alifunga goli dakika ya (73’) kisha kummegea pande zuri Vladlen Yurchenko na kuiandikia goli la tatu Leverkusen dakika ya (88’).Goli la kwanza lilifungwa na Julian Brandt dakika ya 27.
Kufuatia ushindi huo mnono Bayer Leverkusen imefufua matumaini ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao huku wapinzani wao Vfl Wolfsburg wakipoteza matumaini.
VIKOSI
Bayer 04: Leno - Jedvaj, Tah, Ramalho,Wendell - Bender (Chicharito 61’), Kramer -Calhanoglu (Yurchenko 63’), Brandt -Bellarabi, Kießling (Aránguiz 89’)
VfL Wolfsburg: Benaglio - Träsch (Henrique 46’), Knoche (Ascues 83’), Dante, R.Rodriguez- Guilavogui, Arnold - Vieirinha, Draxler,
Schürrle - M.Kruse
0 comments:
Post a Comment