Madrid,Hispania.
Zinedine Zidane amewatema mlinzi Raphael Varane na kiungo Mateo Kovacic katika kikosi cha Real Madrid kilichosafiri kwenda kuivaa Barcelona huko Nou Camp leo saa 21:30.
Bosi huyo wa Los Blancos amemuacha Varane kutokana na kuwa majeruhi huku akishindwa kutoa sababu ya kumuacha Mateo Kovacic na badala yake amewabeba Lucas Vazquez,Jese Rodriguez na mlinzi aliyekuwa majeruhi Sergio Ramos.
Kikosi kamili kilichosafiri ni:
Makipa: Keylor Navas, Kiko Casilla.
Walinzi: Daniel Carvajal, Danilo, Marcelo,Pepe, Nacho Fernandez, Sergio Ramos.
Viungo: Casemiro, Toni Kroos, Luka Modric, Lucas Vazquez, Isco, James Rodriguez.
Washambuliaji: Cristiano Ronaldo, Gareth Bale,Karim Benzema, Jese Rodriguez.
0 comments:
Post a Comment