London,England.
Wakati leo akitarajiwa kucheza mchezo wake wa kwanza akiwa na Chelsea maisha ya mshambuliaji Alexandre Pato ndani ya miamba hiyo ya London yameendelea kuwa magumu.
Taarifa kutoka England zinadai Chelsea imelazimika kushusha bei za jezi namba 11 za nyota huyo wa zamani wa AC Milan baada ya mashabiki kuzikaushia kufuatia raia huyo wa Brazil kushindwa kucheza mchezo hata mmoja tangu aliposajiliwa mwezi Januari.
Bei ya jezi ya blue ambayo hutumika kwa michezo ya nyumbani imeshuka toka £61.95 mpaka £32.87 huku jezi nyeusi ambayo hutumikia kwa michezo ya ya ugenini ikishuka kutoka £51.95 mpaka £27.97.
0 comments:
Post a Comment