Porto,Ureno.
Jose Mourinho ameahidi kumsajili kiungo wake wa zamani katika vilabu vya Chelsea na Real Madrid Mfaransa Lassana Diarra pindi atakapotangazwa kuwa kocha mpya wa Manchester United baadae mwaka huu.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchini Ufaransa hasa Le10Sport ni kwamba Mourinho amevutiwa tena kufanya kazi na Diarra,31 baada ya kiungo huyo wa Marseille kuwa katika kiwango bora sana cha uchezaji msimu huu hali iliyopelekea hata kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa Didier Deschamps amwite katika kikosi chake.
Mbali ya Chelsea na Real Madrid pia Diarra amewahi kuvichezea vilabu vya ligi kuu nchini Uingereza vya Arsenal na Portsmouth.
0 comments:
Post a Comment