Birmingham,England.
Chelsea imeendeleza rekodi yake ya kutopoteza mchezo wowote wa ligi kuu England tangu ilipoanza kunolewa na Guus Hiddink baada ya mchana wa leo kuitandika Aston Villa kwa mabao 4-0 huko Villa Park.
Chelsea ilianza kuandika bao la kuongoza dakika ya 26 kupitia kwa kiungo wake kinda Ruben Loftus-
Cheek kisha ikapata la pili dakika ya 46 kupitia kwa Alexander Pato aliyekuwa ameingia kuchukua nafasi ya Loic Remy aliyeumia.
Pato alifunga bao hilo kwa mkwaju wa penati uliopatikana baada ya kufanyiwa madhambi na mlinzi wa Aston Villa Aly Cissokho.
Mabao mengine ya Chelsea yamefungwa na Pedro Rodriquez dakika za 46 na 59.
Kufuatia ushindi huo Chelsea imechupa mpaka nafasi ya tisa baada ya kufikisha pointi 44 huku Aston Villa ikiendelea kuburuza mkia na pointi zake 16
Aston Villa: Guzan; Hutton, Richards,Lescott, Cissokho; Sanchez, Westwood,
Gueye; Gil, Gestede, Ayew.
Subs: Bunn, Okore, Bacuna, Lyden,Veretout, Grealish, Sinclair.
Chelsea: Courtois; Azpilicueta, Ivanovic,
Miazga, Baba; Mikel, Fabregas; Pedro,
Loftus-Cheek, Kenedy; Remy.
Subs: Begovic, Clarke-Salter, Matic,
Oscar, Traore, Pato, Falcao.
0 comments:
Post a Comment