Lagos,Nigeria.
Nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria na klabu ya Arsenal Nwankwo Kanu ameingia matatani baada ya mahakama ya jiji la Lagos kuamuru akaunti zake zote za benki zifungwe kufuatia kushindwa kulipa mkopo unakaribia kufikia dollar milioni 5 za Marekani (Zaidi ya Naira milioni 924 za Nigeria) anaodaiwa na benki ya Skype.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya benki ya Skype kulifikisha suala hilo mahakamani ikimtuhumu Kanu na kampuni yake ya Hardly Apartments kupiga chenga kulipa mkopo huo waliouchukua kati ya Mei 2008 na Januari 2011 kwa ajili ya biashara ya Hoteli.
Mbali ya kufungwa kwa akaunti zote za mwanasoka huyo wa zamani pia mahakama imeagiza mali zote zinazomilikiwa na hoteli iliyojengwa kwa mkopo huo iliyoko kisiwa cha highbrow Victoria,Lagos ziwe chini ya uangalizi wa muda wa AMCON ( Asset Management Corporation of Nigeria)
0 comments:
Post a Comment