Paul Manjale.
MABINGWA wa soka wa Tanzania Bara,Yanga SC wamepangwa kukutana na miamba wa soka wa Algeria,MC Alger kwenye michezo miwili ya nyumbani na ugenini ya kuwania kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika kwenye droo iliyofanyika mchana wa leo huko Cairo,Misri.
Mouloudia Club d'Alger kwa kifupi inajulikana kama MC Alger MCA.Makao makuu yake yapo Algiers,mji mkuu wa nchi ya Algeria. MC Alger inashiriki ligi daraja la kwanza Algeria maarufu kama Ligue Professionnelle 1.Kwa sasa MC Alger inashika nafasi ya nne kwenye ligi hiyo inayoongozwa na ES Setif.
MC Alger ilianzishwa Agosti 7,1921 ikijulikana kama Mouloudia Chaà bia d'Alger kabla ya mwaka 1977 kubadilishwa jina na kuanza kufahamika kama Mouloudia Pétroliers d'Alger.Jina hilo lilikoma mwaka 1986 na hapo ndipo ilipoanza kuitwa Mouloudia Club d'Alger.Mpaka sasa MC Alger ina umri wa miaka 95.
MC Alger huvalia jezi za rangi nyekundu na kijani na hutumia uwanja wa Stade Omar Hamadi kwa mechi zake za nyumbani.Uwanja huo una uwezo wa kuchukua watazamaji 10,000.
Uongozi: MC Alger iko chini ya mwenyekiti wake Omar Gharib na kocha wake mkuu Kamel Mouassa.Jina la utani la MC Alger ni "The Dean".
MC Alger ndiyo klabu ya kwanza nchini Algeria kutwaa ubingwa wa Afrika hii ni baada ya mwaka 1976 kushinda kombe la klabu bingwa Afrika.
MC Alger ilitwaa ubingwa huo baada ya kuwatwanga mabingwa wa Guinea,Hafia Conakry kwa penati 4-1 baada ya sare ya mabao 3-3 katika michezo miwili ya nyumbani na ugenini. Hafia Conakry ilishinda mabao 3-0 nyumbani na MC Alger nayo ikapata ushindi kama huo nyumbani kwake Stade Omar Hamadi.
Mafanikio
MC Alger ni moja kati ya vilabu vyenye mafanikio makubwa zaidi nchini Algeria.Imeshinda ubingwa wa ligi mara saba (7) hii ikiwa ni 1972, 1975, 1976,
1978, 1979, 1999, 2010.
Ligi ya mabingwa Afrika: 6
1976 – Champion
1977 – Robo fainali
1979 – Raundi ya Pili
1980 – Robo fainali
2000 – Raundi ya Kwanza
2011 – Hatua ya Makundi
Kombe la shirikisho (CAF Confederation Cup): 3
2007 – Raundi ya Kwanza
2008 – Raundi ya Kwanza
2015 – Raundi ya Kwanza
Kombe la washindi (CAF Cup Winners' Cup):Imeshiriki mara moja 1984
na kuishia Raundi ya Pili.
0 comments:
Post a Comment