Mouloude Club de Alger ama Mc Alger ni Moja ya klabu kongwe Algeria iliyoanzishwa mwaka 1921, Wanatumia uwanja wa Omar Hamad uliopo mjini Alger kama uwanja wao wa nyumbani wenye uwezo wa kuchukua mashabiki elfu kumi.
Raisi wao anaitwa Omar Gharib na kocha mkuu wao anaitwa Kamel Moussa
Mafanikio yao makubwa ni kutwaa ubingwa wa vilabu Africa mwaka 1976
Lakini pia wametwaa kombe la ligi kuu Algeria mala saba mwaka 1972,1975,1976,1978,1979,1999 na 2010....Pia wametwaa kombe la Algeria mala 8 mwakq 1971,1973,1976,1983,2006,2007,2014 na 2016 kutwaa kombe hili mwaka Jana ndio kuliwapa nafasi ya kupata uwakili wa Algeria katika mashindano ya caf confederation cup.
Ushiriki wao katika michuano ya CAF na mafanikio yao ni kama ifuatavyo
Klabu Bingwa Africa
1976-Bingwa
1977-Robo fainali
1979-Round ya pili
1980-Robo fainali
2000-Round ya kwanza
2011-Hatua ya makundi
Caf confederation cup
2007-Round ya kwanza
2008-Round ya kwanza
2015-Round ya kwanza
Algeria ni Moja ya nchi inayotoa washiriki wanne katika michuano ya Africa ambapo klabu bingwa wawakilishi wawili na kombe la shirikisho wawili, Mc Alger alipata nafasi baada ya kua mshindi wa kombe la algeria .
Kufikia hatua hii ya play off katika mashindano haya ya Caf ,Mc Alger walianza hatua ya awali yaani preminary round kwa kucheza na timu ya Bechem United toka Ghana, mechi ya awali walicheza Ghana ambapo Bechem united iliibuka na ushindi wa goli mbili kwa Moja ,mechi ya marudiano Mc Alger walishinda goli NNE kwa Moja hivyo kufuzu kwa jumla ya magoli Matano kwa Matatu ya Bechem, Baada ya kufuzu hatua ya awali walipangiwa timu ya Rennaisance du Congo toka DRC katika first round stage , mechi ya kwanza ilichezwa Algeria ambapo Mc Alger walishinda goli mbili kwa bila na mechi ya marudiano iliyofanyika Congo Dr walipigwa goli mbili kwa Moja hata hivyo walifuzu kwa jumla ya magoli matatu kwa mawili, hawa ndio wapinzani wa Yanga.
0 comments:
Post a Comment