Wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya Afrika, Yanga kufahamu wamepangwa na klabu gani katik hatua ya mchujo wa mwisho wa kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho itakatwa leo mchana.
Shirikisho la Soka Afrika, CAF linatarajiwa kufanya droo ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika na ile ya mchujo wa mwisho wa kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shrikisho hii leo.
Tayari timu za Ligi ya Mabingwa zimegawanywa katika makundi manne kulingana na viwango vyao wakati timu 32 za Kombe la Shirikisho zikigawanywa katika makundi mawili.
Yanga iliangukia katika Kombe la Shirikisho baada ya kutolewa na Zanaco ya Zambia katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa sheria ya bao la ugenini.
0 comments:
Post a Comment