728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, March 21, 2017

    Ronaldo mchezaji bora wa mwaka Ureno,

    Lisbon,Ureno.

    STAA wa Real Madrid,Cristiano Ronaldo ameendelea kujikusanyia tuzo kila inapoitwa leo baada ya usiku wa kumkia leo kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2016 nchini kwake Ureno.

    Ronaldo,32,ameibuka mshindi baada ya mwaka 2016 kuiongoza Ureno kutwaa ubingwa wake wa kwanza wa Ulaya huku pia akiiongoza Real Madrid kushinda ubingwa wake wa kumi na moja (11) wa michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya akiibuka mfungaji bora baada ya kufunga mabao 16.

    Ronaldo ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwabwaga wapinzani wake wa karibu  beki wa Real Madrid,Pepe pamoja na kipa wa Sporting Lisbon,Rui Patricio.


    Kiungo wa Bayern Munich, Renato Sanches,ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka kijana.Fernando Santos ametwaa tuzo ya kocha bora wa mwaka baada ya mwaka 2016 kuiongoza Ureno kutwaa ubingwa wake wa kwanza wa Ulaya.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Ronaldo mchezaji bora wa mwaka Ureno, Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top