Chicago,Marekani.
KIUNGO wa Manchester United na mshindi wa kombe la dunia la mwaka 2014,Mjerumani Bastian Schweinsteiger amejiunga na klabu ya Chicago Fire inayoshiriki ligi kuu ya nchini Marekani.
Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye gazeti la Chicago Tribune, Schweinsteiger amejiunga na Chicago Fire kwa mkataba wa mwaka mmoja na atakuwa akilipwa mshahara wa Dola Milioni 4 kwa mwaka.
Akithibisha taarifa hizo Mkurugenzi wa Chicago Fire,Nelson Rodriguez amesema "Tunamuongeza mtu ambaye ameshinda mataji katika kila hatua (level) ikiwemo hatua ya juu kabisa tena katika namna inayowoana na mahitaji yetu.
Schweinsteiger alijiunga na Manchester United mwaka 2015 akitokea Bayern Munich lakini amejikuta alicheza michezo 18 pekee baada ya msimu uliopita kutibuana na Kocha Jose Mourinho.
Schweinsteiger anakuwa mchezaji wa tano kujiunga na Chicago Fire msimu huu.Wengine ni David Accam,Nemanja Nikolic,Dax McCarty na Juninho.
0 comments:
Post a Comment