Frankfurt, Ujerumani.
KOCHA wa Hoffenheim Julian Nagelsmann,kocha mdogo zaidi kwenye historia ya ligi ya Bundesliga,jana Jumatatu usiku aliibuka kidedea baada ya kutwaa tuzo ya kocha bora wa mwaka 2016.
Nagelsmann,29,ametwaa tuzo hiyo baada ya msimu uliopita akiwa na kikosi kilichojaa vijana wadogo kabisa kuiondoa Hoffenheim kwenye hatari ya kushuka daraja na kuibakiza Bundesliga.
Msimu huu Hoffenheim chini ya Nagelsmann, inashikilia nafasi ya nne Bundesliga.Nafasi ambayo itaipatia klabu hiyo tiketi ya kushiriki hatua ya mtoano ya kuwania kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya klabu bingwa Ulaya.
Mkurugenzi wa michezo wa shirikisho la soka la Ujerumani,Horst Hrubesch amesema Nagelsmann ni mfano mzuri wa vipaji lukuki vya makocha ambavyo nchi hiyo imejaaliwa kuwa navyo.
0 comments:
Post a Comment