Manchester,England.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Daily Mirror zinasema kwamba Jose Mourinho atakuwa mbele ya mstari kama mshambuliaji Romelu Lukaku ataondoka Everton.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ubeligiji wiki iliyoipita aliongea kuhusu nia yake ya kutaka kucheza mashindano ya UEFA, na huenda akawa mbadala wa Zlatan Ibrahimovic katika kikosi cha United.
Mourinho pia anataka kuimarisha nafasi ya beki wa pembeni na jicho lake limetua kwa beki wa kulia wa Benfica, Nelson Semedo.Beki huyo wa kimataifa wa Ureno amehusishwa pia na vilabu vya AC Milan na Juventus.
0 comments:
Post a Comment