Barcelona,Hispania.
Taarifa ya usajili kutoka Hispania, jarida la Mundo Deportivo limearifu kwamba Barcelona wameonesha nia ya kutaka kuwasajli Marco Verratti na Phillipe Coutinho.
Verratti ana mkataba na Paris St-Germain mpaka mwaka 2020 na Coutinho pia mapema mwaka huu alisaini mkataba mpya katika klabu ya Liverpool mpaka mwaka 2022.Lakini Barca wanataka kusajili mmoja wa viungo hao kwa mujibu wa Mundo Deportivo.
0 comments:
Post a Comment