Barcelona,Hispania.
Nyota wa kimataifa wa Brazil anayekipaga Barcelona,Neymar Jr,ameweka wazi kwamba anatamani siku moja akipige ligi kuu ya Uingereza.
Neymar Jr aliliambia gazeti la The Sun ," Ligi kuu ya Uingereza ni ligi ambayo inanivutia sana."
"Napenda aina ya uchezaji wao na timu zao pia.Na nani anajua, siku moja ningependa kucheza Uingereza, bila shaka."
"Nazikubali Manchester United, Chelsea, Arsenal na Liverpool - hivi ni vilabu ambavyo kila msimu vinapigania ubingwa."
"Halafu pia kuna makocha wa kiwango cha juu sana, Jose Mourinho na Pep Guardiola. Hawa ni aina ya makocha ambao mchezaji unatamani kufanya nao kazi."
0 comments:
Post a Comment