Madrid,Hispania.
Antoine Griezmann amesema kwamba ana furaha katika klabu yake ya Atletico Madrid na amesisitiza kwamba mustakabali wake upo mikononi mwa klabu.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa ameripotiwa kuwindwa na klabu ya Manchester United.
Griezmann alisema jana," Nimeshasema sana hapo nyuma, nina mkataba na Atletico Madrid na nina furaha hapa pamoja na Familia yangu."
"Na hata hivyo, kuondoka hapa, itatakiwa klabu itake kuniuza mimi au sio ? "
"Najaribu kuwa na furaha nikiwa uwanjani na kuisaidia klabu kupata matokeo. kila kitu kinaenda sawa. Hapa jua linatoka mwaka mzima na hiyo pia inasaidia."
0 comments:
Post a Comment