Jeju,Korea Kusini.
DROO ya upangaji wa makundi ya michuano ya kombe la dunia la FIFA la vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 (U-20) imefanyika mchana wa leo huko Jeju,Korea Kusini ambapo jumla ya mataifa 24 yamepangwa katika makundi sita (6) ya timu nne nne.
Katika droo hiyo iliyoendeshwa na nyota wa zamani wa Argentina,Diego Maradona mshindi wa kombe hilo la mwaka 1979 pamoja na Pablo Aimar mshindi wa kombe hilo la mwaka 1997 imeishuhudia mabingwa wa Afrika, Zambia wakipangwa kundi C pamoja na mabingwa mara mbili wa michuano hiyo Ureno, Iran, Costa Rica.
Wawakilishi wengine wa Afrika kwenye michuano hiyo,Senegal wao wamepangwa kundi F pamoja na mataifa ya Marekani, Ecuador na Saudi Arabia.
Michuano hiyo itafanyika katika miji sita ya Cheonan, Daejeon, Incheon, Jeju,Jeonju na Suwon kuanzia Mei 20 na kufikia tamati Juni 11.
Timu mbili za juu kutoka kila kundi vitaungana na timu nne zitakazokuwa zimeshika nafasi ya tatu kufuzu hatua ya 16 bora itakayochezwa Mei 30, Mei 31 na Juni 1.
Droo Kamili
Kundi A: Korea Republic, Guinea, Argentina,
England
Kundi B: Venezuela,Germany, Vanuatu,Mexico
Kundi C: Zambia, Ureno, Iran, Costa Rica
Kundi D: South Africa,Japan, Italy, Uruguay
Kundi E: France, Honduras, Vietnam, New Zealand
Kundi F: Ecuador, USA, Saudi Arabia, Senegal
0 comments:
Post a Comment