728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, March 16, 2017

    Bao la ugenini laipeleka Monaco robo fainali ligi ya mabingwa Ulaya

    Monaco,Ufaransa.

    Monaco ikiwa nyumbani Stade Louis II imeichapa Manchester City mabao 3-1 kwenye mchezo wa marudiano wa hatua ya 16 bora na kutinga robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

    Mpaka mapumziko wenyeji Monaco walikuwa mbele kwa mabao ya mshambuliaji kinda,Mbappe Lottin pamoja na mlinzi wa kulia Fabinho.

    Kipindi cha pili Manchester City walijitutumua na kufanikiwa kupata bao kupitia kwa kiungo wake Leroy Sane lakini bao hilo halikusaidia sana kwani Monaco waliongeza bao la tatu kupitia kwa kiungo wake Tiomoue Bakayoko.

    Ikumbukwe kwenye mchezo wa awali Monaco ilifungwa mabao 3-2 huko Manchester hivyo ushindi wake wa leo Jumatano umeifanya miamba hiyo ya Ufaransa itinge robo fainali kwa faida ya bao la ugenini baada ya matokeo ya jumla kuwa mabao 6-6.

    VIKOSI
    Monaco: Subasic, Sidibe, Raggi,Jemerson, Mendy, Fabinho, Bakayoko,Lemar, Bernardo Silva, Germain,Mbappe-Lottin.

    Man City: Caballero, Sagna, Stones,Clichy, Kolarov, Sane, Fernandinho, Silva,De Bruyne, Aguero, Sterling.

    Mwamuzi: Gianluca Rocchi (Italia)



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Bao la ugenini laipeleka Monaco robo fainali ligi ya mabingwa Ulaya Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top