Addis Ababa,Ethiopia.
SHIRIKISHO la vyama vya soka Afrika (CAF) limevitangaza rasmi viwanja viwili ya Franceville na Port Gentil iliyoko nchini Gabon kuwa ndiyo itakayokuwa viwanja wenyeji wa michuano ya mwaka huu ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ambapo Tanzania itawakilishwa na Serengeti Boys.
Viwanja hiyo vimetangazwa jana Jumanne usiku kwenye mkutano mkuu wa 39 wa CAF unaoendelea huko Addis Ababa,Ethiopia kujadili mambo mbalimbali ikiwemo kumsaka Rais mpya wa shirikisho hilo kupitia uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika kesho Alhamis.
Awali michuano hiyo ilipangwa kufanyika Madagascar kati ya Aprili 2-16 lakini CAF ikaamua kuupiga chini mpango huo na Februari 3 mwaka huu ikatangaza kuipa wenyeji nchi ya Gabon na michuano hiyo kupangwa kufanyika kati ya Mei 21-Juni 4.
Uwanja wa Stade de Port-Gentil ulioko kwenye mji wa Port-Gentil una uwezo wa kuchukua watazamaji 20,000 wakati uwanja Stade de Franceville ulioko kwenye mji wa Franceville wenye una uwezo wa kuchukua watazamaji 22,000.Hii ina maana kwamba Serengeti Boys itacheza michezo yake kwenye moja kati ya viwanja hivyo.
Timu nne za juu kati ya Angola,Cameroon, Gabon, Ghana, Guinea, Mali,Niger na Tanzania zitafuzu fainali ya kombe la dunia la vijana litakalofanyika mwaka huu huko nchini India.
0 comments:
Post a Comment