Dar es salaam,Tanzania.
SHIRIKISHO la soka Tanzania (TFF) limekubali kuisogeza mbele mechi ya
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya mabingwa watetezi, Yanga
dhidi ya Mtibwa Sugar iliokuwa ichezwe Jumatano (Aprili 6, 2016) na badala yake itapigwa Aprili 16 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Hiyo inafuatia malalamiko ya Yanga kupangiwa mechi tatu ndani ya wiki moja kabla ya kumenyana na Al Ahly ya Misri Jumamosi ijayo katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
0 comments:
Post a Comment