Turin,Italia.
Juventus imejisogeza karibu kabisa na ubingwa wa tano mfululizo wa Scudetto (Seria A) baada ya jumamosi usiku kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Empoli.
Bao pekee la mchezo huo uliopigwa katika dimba la Juventus Arena limefungwa dakika ya 44 na mshambuliaji Mario Mandzukic.
Mandzukic alifunga bao hilo kwa kichwa akiunganisha pasi nzuri ya kiungo Paul Pogba na kufuta ukame wa kucheza miezi mitatu bila ya kufunga bao.
Kufuatia ushindi huo Juventus imefikisha pointi 73 baada ya kushuka dimbani mara 31 huku nafasi ya pili ikikaliwa na Napoli yenye 67 huku ikiwa na mchezo mmoja pungufu.
Ligi hiyo itaendelea tena leo jumapili kwa michezo mitatu:Udinese itakuwa mwenyeji wa Napoli,Lazio v Roma wakati Torino ikiitembelea Inter Milan.
0 comments:
Post a Comment