728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, April 03, 2016

    EL CLASICO:RONALDO AITUNGUA BARCA NA KUIREJESHA REAL MADRID KATIKA MBIO ZA UBINGWA

    Barcelona,Hispania.

    Real Madrid imefufua matumaini ya kutwaa ubingwa wa La Liga baada ya jumamosi usiku kuitandika Barcelona kwa mabao 2-1 katika mchezo mkali na wa kusisimua uliopigwa katika dimba la Nou Camp,Barcelona.

    Katika mchezo huo uliotawaliwa na kashikashi za hapa na pale toka kwa wachezaji wa pande zote mbili na kupelekea mlinzi wa Real Madrid Sergio Ramos kuliwa kadi nyekundu.

    Wenyeji Barcelona ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 56 lililofungwa kwa kichwa na mlinzi Gerrard Pique 56 akiunganisha kona ya kiungo Ivan Rakitic.

    Kuingia kwa bao hilo kuliiamsha Real Madrid iliyokuja juu na kusawazisha dakika ya 62 kupitia kwa Karim Benzema.

    Mchezo ukiwa unaelekea mwishoni Cristiano Ronaldo aliipatia Real Madrid bao la ushindi dakika ya 85 akimalizia kazi nzuri ya Gareth Bale aliyeambaa na mpira na kutoa krosi nzuri na kuzima rekodi ya Barcelona ya kucheza michezo 39 bila kufungwa.

    Kufuatia ushindi huo Real Madrid imefanikiwa kufikisha pointi 69 pointi 7 nyuma ya Barcelona yenye pointi 76 huku kila timu ikibaki na michezo sita.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: EL CLASICO:RONALDO AITUNGUA BARCA NA KUIREJESHA REAL MADRID KATIKA MBIO ZA UBINGWA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top