London,England.
Wakati Arsenal ikilipa kisasi kwa kuitandika Watford 4-0 jana jumamosi nyumbani Emirates kiungo wake Mmisri Mohamed Elneny aliweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyepiga pasi nyingi zaidi katika mchezo mmoja kupita wachezaji wote wanaokipiga ligi kuu England msimu wa 2015/16.
Elneny,23 ambaye alijiunga na Arsenal mwezi Januari mwaka huu akitokea FC Basel kwa kitita cha paundi milioni 5 katika mchezo dhidi ya Watford alifanikiwa kupiga pasi 121 na kuipiku rekodi ya pasi 120 iliyokuwa ikishikiliwa na nyota mwenzie wa Arsenal Santi Cazorla.
Hii hapa orodha ya wachezaji wanaoongoza kwa kupiga pasi nyingi zaidi katika mchezo mmoja wa ligi kuu England.
1. Mohamed Elneny vs Watford – 121 passes
2. Santi Cazorla vs Newcastle – 120 passes
3. Fernandinho vs Norwich – 116 passes
4. Cesc Fabregas vs Southampton – 112 passes
5. Santi Cazorla vs West Brom – 111passes
0 comments:
Post a Comment