Yanga SC inakusudia kuhamishia mechi zake za kimataifa kwenye uwanja wa CCM kirumba Mwanza madai kwamba makelele ya mashabiki wa Simba yanawazingua wachezaji wao Jijini Dar es salaam '
Yanga wanadai kwamba wachezaji wamekuwa hawana uhuru wanapokuwa uwanja wa Taifa lakini wanapokuwa ugenini wanacheza kwa kiwango cha juu zaidi '
Mjumbe wa kamati ya Mashindano ya Yanga Samuel Lukumay ambaye aliiongoza Yanga kwenda Zambia pamoja na staa wa timu hiyo Simon Msuva wamesisita kwamba sasa imetosha ni bora Yanga ihamie Mwanza na mashabiki wao wataifuata hukohuko.
0 comments:
Post a Comment