London,England.
UMESIKIA!!ARSENE Wenger anatarajia kubakia Arsenal kwa kipindi cha mwaka mmoja zaidi licha ya mashabiki wa klabu hiyo kuanzisha kampeni kali kuhakikisha kocha huyo ananyimwa mkataba mpya pindi ule wa sasa utakapokwisha mwishoni mwa msimu huu.
Hivi karibuni Arsenal imepoteza michezo yake minne kati ya mitano iliyopita ya ligi kuu England huku ikitolewa kwa mara ya saba mfululizo kwenye hatua ya 16 ya michuano ya klabu bingwa Ulaya hali ambayo imefanya mashabiki wa klabu hiyo waanze kumwandama Wenger na mabango yenye jumbe kama "Hakuna Mkataba Mpya",Mwisho Umefika na kadharika.
Lakini taarifa za leo hii kutoka gazeti la The Express zimesema Wenger na wakuu wa Arsenal tayari wameshafikia makubaliano kuwa atasalia klabuni hapo kwa mwaka mmoja zaidi.
Taarifa zaidi zinasema awali Arsenal ilitaka kumpa Wenger mkataba wa miaka miwili lakini kocha huyo kwa kutambua hasira kali za mashabiki wa klabu hiyo ameamua kusalia Emirates kwa miezi 12 pekee.
Wenger, 67,amedumu Arsenal kwa miaka 21 tangu alipochukua mikoba ya kocha George Graham mwaka 1996 akitokea Nagoya-Japan.
0 comments:
Post a Comment