Barcelona,Hispania.
LIONEL MESSI ameendelea kuvunja rekodi za wenzake na kuweka za kwake baada ya jana Jumapili kuifungia Barcelona mabao mawili na kuiwezesha kuitwanga Valencia mabao 4-2 nyumbani Camp Nou.
Mabao hayo mawili yamemfanya Messi ,29, kuweka rekodi mbili kubwa nchini Hispania.
Kwanza yamemfanya kuwa mchezaji pekee anayechezea ligi ya La Liga kufikisha mabao 40 katika micheano yote ndani ya misimu minane mfululizo iliyopita.
Pili mabao hayo yamemfanya Messi kuwa mchezaji wa kwanza kufunga zaidi ya mabao 25 kwenye ligi ya La Liga katika misimu minane mfululizo iliyopita.Mpaka sasa Messi amefunga mabao 41katika michezo 40 ya michuano yote.
0 comments:
Post a Comment