Dar Es Salaam,Tanzania.
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania anayecheza soka ya kulipwa nchini Sweden kwenye klabu ya AFC Eskilstuna,Thomas Ulimwengu hatajiunga na kikosi Taifa Stars kinachojiandaa kucheza michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa hivi karibuni.
Taarifa ambayo imetolewa na Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Alfred Lucas imesema Ulimwengu hatakuwa sehemu ya kikosi cha Taifa Stars kwa kuwa
hayuko fiti kutokana na kusumbuliwa na majeruhi na sasa yuko chini ya uangalizi wa madaktari wa klabu hiyo.Hivyo kuja kwake kuitumikia Taifa Stars kutaharibu programu nzima ya tiba.
Taifa Stars inatarajiwa kucheza na Botswana Machi 25,kabla ya kuivaa Burundi Machi 28,mwaka huu katika michezo ya kimataifa ya kirafiki inayotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
0 comments:
Post a Comment