728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, March 06, 2017

    Kenya yatamba mchezo wa judo Zanzibar,Bongo yatia aibu


    Lameck Francis
    Zanzibar.

    Mashindano ya 11 ya Judo ya Afrika Mashariki na Kati yaliyofanyika kwa siku mbili yamemalizika jana jioni katika Ukumbi wa Judo uliopo Aman Mjini Unguja ambapo Kenya wameongoza na Burundi wakishika nafasi ya pili pia wenyeji Zanzibar kukamata nafasi ya tatu na bongo kuburuta mkia.

    Kenya imeongoza ikishinda Medali za dhahabu (Gold) 4, Fedha (Silver)1 na Shaba (Bronze) 8 huku Burundi ikishika nafasi ya pili baada ya kushinda Medali za Dhahabu 3, Fedha 3 na Shaba 2 huku wenyeji wa Mashindano hayo Zanzibar ikishika nafasi ya tatu baada ya kupata Medali ya Dhahabu 1, Fedha 2 na Shaba 2 na timu ya mwisho katika Mashindano hayo ni Tanzania Bara waliyoambulia Medali moja ya Fedha na moja ya Shaba.

    Burundi ambao wamekamata nafasi ya pili wachezaji wao walioshinda Medali za Dhahabu kwa Wanaume ni Samuel Kwitonda uzito wa kilo 81 na kwa upande wa Wanawake ni Angeciella Niragira uzito wa kilo 70 pamoja na Enia Irakole kilo 78 wakati Zanzibar alipata Medali ya Dhahabu ni Masoud Amour Kombo pekee aliyeshinda kwenye uzito wa kilo 100 hii ni mara yake ya 10 mfululizo kushinda katika mashindano hayo.Mashindano hayo yatafanyika tena mwakani kwa mara ya 12 ambapo kenya ndio watakao kuwa wenyeji
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Kenya yatamba mchezo wa judo Zanzibar,Bongo yatia aibu Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top