London,England.
Klabu ya West Ham United inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza imesitisha mpango wa kuwasajili moja kwa moja nyota watatu wa Afrika waliopo klabuni hapo kwa mkopo Alex Song,Victor Moses na Emmanuel Emenike .
Sababu inayodaiwa kuifanya Westham United iamue kuachana na mpango huo licha ya mwanzo kuonyesha nia ya kuendelea kuwa na wachezaji hao msimu ujao ni kuwa Song na wenzake wameshindwa kupata namba katika kikosi cha kwanza cha Slaven Bilic.
Sababu nyingine iliyotolewa ni kuwa Song na Victor Moses wamekuwa majeruhi kwa kipindi kirefu hivyo kushindwa kuisaidia klabu vya kutosha.Emenike amedaiwa kukosa kasi ya kufumania nyavu.
Hii ina maana kwamba mwisho wa msimu Song atarejea Barcelona, Moses-Chelsea na Emenike atarudi zake Al Ain.
0 comments:
Post a Comment