728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, April 05, 2016

    AL AHLY YAJA NA NYOTA 22 KUIVAA YANGA JUMAMOSI,YUMO NA ALIYEITOA NIGERIA AFCON

    Ramadan Sobhy kiungo aliyeiua Nigeria AFCON


    Na Paul Manjale

    Cairo,Misri.

    Kocha mkuu wa Al Ahly Mholanzi Martin Jol ametangaza kikosi cha wachezaji 22 kitakachokuja kuvaana na Yanga katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya 16 bora ya michuano ya vilabu bingwa Afrika jumamosi hii katika dimba la Uwanja wa Taifa,Dar es salaam.

    Pia Jol amewatema kikosini beki Mohamed Naguib na viungo Saleh Gomaa na 
    Ahmed Hamdy kwa sababu zinazodaiwa kuwa ni za kiufundi huku mlinzi wa kushoto Hussein El-Sayed akibaki kulitumikia jeshi kama sheria za nchi hiyo zinavyoagiza.

    Kikosi kamili cha Al Ahly kinachotarajiwa kuondoka Cairo jumanne ya leo ni pamoja na:

    Makiba: Sherif Ekramy, Ahmed Adel na Mosaad Awad.

    Walinzi: Ahmed Fathi, Bassem Ali,Mohamed Hani, Saad Samir, Rami Rabia,
    Ahmed Hagazy na Sabry Rahil.

    Viungo: Hossam Ghaly, Hossam Ashour, Amr El-Sulaya, Ahmed El-Sheikh,
    Walid Soliman, Momen Zakaria, Ramadan Sobhy na Abdallah El-Said.

    Washambuliaji: Malick Evouna, Amr Gamal, John
    Antwi na Emad Meteb.

    Yanga na Al Ahly zitavaana jumamosi ya April 9 jijini Dar es salaam na kisha kurudiana tena siku kumi baadae jijini Cairo.

    Al Ahly imefanikiwa kutinga hatua ya16 bora baada ya kuiondoa Recreativo ya Angola kwa jumla ya mabao 2-0 huku Yanga ikitinga hatua hiyo kwa kupata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya APR ya Rwanda.

    Mchezo wa jumamosi utakuwa unazikutanisha Yanga na Al Ahly mara ya pili katika kipindi kisichozidi miaka miwili.Timu hizi zilikutana mwaka 2014 na Al Ahly kuibwaga Yanga kwa mikwaju ya penati baada ya matokeo ya jumla ya bao 1-1.





    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: AL AHLY YAJA NA NYOTA 22 KUIVAA YANGA JUMAMOSI,YUMO NA ALIYEITOA NIGERIA AFCON Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top