Alex Iwobi
London,Uingereza.
ULAJI!!Arsenal imemzawadia kinda wake Mnigeria Alex Iwobi mkataba mpya wa miaka mitano baada ya kuridhishwa na maendeleo yake tangu alipoanza kukitumikia kikosi cha wakubwa.
Mkataba huo mpya utakaofikia mwisho mwaka 2021 utamuwezesha Iwobi,19, kuvuna mshahara wa paundi 30,000 kwa wiki hii ikiwa ni ongezeko la paundi 20,000 toka katika mkataba wa awali wa paundi 10,000 aliousaini mwezi Oktoba mwaka Jana.
Alex Iwobi ni mpwa wa nyota wa zamani wa Nigeria na Bolton Wanderers Jay jay Okocha.Iwobi amefanikiwa kuifungia Arsenal mabao mawili mpaka sasa katika michezo ya ligi kuu dhidi ya Everton na Watford.
0 comments:
Post a Comment