728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, April 06, 2016

    LIGI YA MABINGWA ULAYA:SUAREZ APIGA MBILI,BARCELONA IKIICHAPA ATLETICO MADRID 2-1 NOU CAMP

    Barcelona,Hispania.

    Mabao mawili ya kipindi cha pili ya mashambuliaji Luis Suarez yameiwezesha Barcelona kutoka nyuma na kuichapa Atletico Madrid 2-1 katika mchezo wa kwanza wa hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya huko Nou Camp jana jumanne usiku.

    Walikuwa ni wageni Atletico Madrid ndio walioanza kuandika bao mapema dakika ya 25 ya kipindi cha kwanza kupitia kwa mshambuliaji Fernando Torres ambaye baadae dakika ya 35 alilimwa kadi nyekundu na mwamuzi Felix Brych baada ya kumchea rafu kiungo wa Barcelona Sergio Busquets. 
    Mpaka mapumziko matokeo yalikuwa Barcelona 0-1 Atletico Madrid.

    Kipindi cha pili Barcelona ilitumia vyema mwanya wa wapinzani wao kuwa pungufu kwa kufanya mashambulizi mengi na kufanikiwa kupata bao dakika ya 63 kupitia kwa Luis Suarez.

    Dakika ya 74 Suarez tena aliipa uongozi Barcelona baada ya kuifungia bao safi kwa kichwa akiunganisha krosi ya murua ya mlinzi Dani Alves aliyepanda kusaidia mashambulizi.

    Timu hizo zitajitupa tena uwanjani April 13 huko Vicente Calderon jijini Madrid na mshindi atatinga hatua ya nusu fainali.






    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: LIGI YA MABINGWA ULAYA:SUAREZ APIGA MBILI,BARCELONA IKIICHAPA ATLETICO MADRID 2-1 NOU CAMP Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top