Napoli,Italia.
Mshambuliaji wa Napoli Muargentina Gonzalo Higuain anakabiliwa na adhabu ya kufungiwa michezo mitatu ya ligi ya Seria A kufuatia kumfanyia fujo mwamuzi Massimiliano Irrati akipinga kadi nyekundu aliyoonyeshwa kwa mchezo mbaya.
Higuain,28 alionyeshwa kadi ya pili ya njano kisha nyekundu baada ya kumkwatua kwa nyuma mlinzi wa Udinese Felipe huko Estadio Friuli.
Baada ya kadi hiyo Higuain alicharuka na kumsukuma mwamuzi Massimiliano Irrati kabla ya kutolewa kwa nguvu uwanjani na wachezaji wenzake wa Napoli.
Katika mchezo huo Napoli ililala kwa mabao 3-1 toka kwa Udinese inayopambana kujinasua toka mkiani mwa ligi ya Seria A.
Kwa mujibu wa sheria za soka la Italia mchezaji yeyote atakayemfanyia fujo mwamuzi atakabiliwa na adhabu ya kufungiwa michezo isiyopungua mitatu.
0 comments:
Post a Comment