728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, April 04, 2016

    ANTONIO CONTE MENEJA MPYA CHELSEA

    London,England.

    Klabu ya Chelsea imemtangaza Muitaliano Antonio Conte kuwa kocha wake mpya akichukua mikoba ya Jose Mourinho aliyetimuliwa kazi Disemba mwaka jana.

    Conte ametambulishwa leo mbele ya waandishi wa habari baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu wa kuifundisha miamba hiyo ya Stamford Blidge.

    Conte,46,ambaye kwa sasa anakinoa kikosi cha Italia anakuwa Muitaliano wa tano kuifundisha Chelsea baada ya Gianluca Vialli, Claudio Ranieri,Carlo Ancelotti na Roberto Di Matteo huku akiwa ni kocha wa nane wa kudumu tangu bilionea Roman Abramovich aanze kuimiliki Chelsea miaka 13 iliyopita.

    Historia yake kwa Ufupi!!

    Akiwa kama mchezaji wa kiungo!!Antonia Conte alifanikiwa kuichezea Juventus zaidi ya michezo 400 akiisaidia kutwaa mataji matano ya Seria A na moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

    Alifanikiwa kuichezea Italia michezo 20.Mwaka 2000 Conte alikuwa sehemu ya kikosi cha Italia kilichofungwa na Ufaransa katika mchezo wa fainali ya Euro uliofanyika Uholanzi.

    Akiwa kama kocha!! 

    Conte alifanikiwa kuiongoza Juventus kutwaa mataji matatu mfululizo ya Serie A hiyo ikiwa ni mwaka 2012 mpaka 2014.





    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ANTONIO CONTE MENEJA MPYA CHELSEA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top