Milan,Italia.
Mario Balotelli anajuta kuitosa Ghana na kuchagua kuichezea Italia,hii ni kwa mujibu wa baba mzazi wa nyota huyo wa Liverpool.
Thomas Barwuah,ambaye ni baba mzazi wa amefichua kuwa ubaguzi pamoja mdomo wa vyombo vya habari vya Italia vimemfanya mwanae ajutie kuitosa Ghana.
Akiongea na GazzettaGhana,Barwuah amesema
“Balotelli amewaambia mara kadhaa marafiki zake kuwa anajuta kuchagua kuchezea timu ya taifa ya Italia badala ya taifa lake la asili Ghana.
“Waitaliano hawamjali,hawamwonyeshi upendo anaostahili kutokana na kuwa na kipaji kikubwa cha kucheza soka.
"Anachopata kutoka kwao ni matusi tu hasa kutoka kwa vyombo vya habari na hii ni kwa sababu yeye ni mtu mweusi.
“Hawampendi na hii ilianza tangu mwanzo.Hawakutaka kuona kijana mweusi kama yeye akiichezea timu ya taifa ya Italia".Alimaliza Barwuah.
Balotelli alikataa kuichezea Ghana mwaka 2011 licha ya maofisa wa chama cha soka cha Ghana kumbembeleza mara kadhaa akubali kuichezea Black Stars.Balotelli alikataa akisisitiza kuwa amekulia Italia,yeye ni Muitalia na ataichezea Italia (Azurri).
Mwaka 2012 Balotelli aliipeleka Italia katika fainali ya Euro baada ya kuifungua mabao mawaili katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Ujerumani kabla ya kupoteza mchezo wa fainali kwa kuchapwa na Hispania 4-1.
0 comments:
Post a Comment