London,England.
Chama cha soka cha England FA leo kimetangaza majina sita ya wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa ligi kuu ya England. maarufu kama PFA Players' Player of the Year award.
Katika orodha ya tuzo hiyo inayojulikana kama PFA Players' Player of the Year award vinara wa ligi kuu ya England Leceister City wameendelea kutamba baada ya kuingiza wachezaji watatu katika kinyang'anyiro hicho.
Orodha kamili iko kama ifuatavyo!!
Jamie Vardy,N'Golo Kante na Riyad Mahrez (Leceister City),Dimitri Payet (Westham United),Harry Kane (Tottenham) na Mesut Ozil (Arsenal).Tuzo hiyo msimu uliopitwa ilitwaliwa na winga wa Chelsea Eden Hazard.
Orodha ya wanaowania tuzo ya mchezaji bora kijana ni:
Harry Kane na Dele Alli (Tottenham),Romelu Lukaku na Ross Barkley (Everton),Jack Butland (Stoke City) na Philippe Coutinho (Liverpool).Tuzo hii ilitwaliwa na Harry Kane msimu uliopita.
Washindi wa tuzo hizo watatangazwa jumapili ya April 24 mwaka huu.
Kwa upande wa ligi ya wanawake wanaowania tuzo hiyo ni:
Mchezaji bora wa msimu uliopita Ji So-Yun anawania tena akiwa na wachezaji wenzie wa Chelsea Hedvig Lindahl na Gemma Davison,Izzy Christiansen (Manchester City) na Beth Mead (Sunderland)
Wanaowania tuzo ya wachezaji vijana kwa upande wa wanawake ni:
Beth Mead (Sunderland),Nikita Parris na Keira Walsh (Manchester City) ,Hannah Blundell (Chelsea) na Danielle Carter (Arsenal)
Washindi wa tuzo hizo watatangazwa jumapili ya April 24 mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment