Barcelona,Hispania.
NYOTA watatu wa Barcelona,Andres Iniesta,Ivan Rakitic na Gerard Pique wamemtaja Kocha msaidizi wa klabu hiyo, Juan Carlos Unzue kuwa ndiye mtu sahihi wa kuvaa viatu vya kocha mkuu wa sasa, Luis Enrique anayeachia ngazi mwishoni mwa msimu huu.
Wachezaji hao wamesema hayo kupitia Radio Cadena Ser kuwa Unzue,49, anaijua vyema Barcelona kwani amekuwa klabuni hapo kwa kipindi kirefu akihudumu kama mchezaji na baadae kama kocha wa makipa hivyo kuvaa viatu vya Enrique haitakuwa kazi ngumu kwake na badala yake itakuwa rahisi kama kumsukuma mlevi vile.
Unzue ni mmoja kati ya makocha wawili wanaotazamwa kwa karibu kuchukua mikoba ya Enrique.Mwingine ni kocha wa Atletic Bilbao,Ernesto Valverde.
Unzue amehudumu Barcelona akiwa mchezaji mwaka 1988-90,kocha wa makipa kutoka mwaka 2003-10 kisha akarejea tena mwaka 2011-12 akitokea Numancia alikokwenda kuhudumu kama kocha mkuu.
Mwaka 2013 Unzue alikuwa msaidizi wa Enrique Celta Vigo kabla ya 2014 wawili hao kutua Barcelona na kufanikiwa kutwaa vikombe kumi mpaka sasa.
0 comments:
Post a Comment