728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, March 18, 2017

    Aubameyang afikisha mabao 23 Bundesliga, Dortmund ikiinyuka Ingolstadt (+ Video)


    Dortmund,Ujerumani.

    Pierre-Emerick Aubameyang (Pichani) akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kuifungia Borussia Dortmund bao pekee katika ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wachovu Ingolstadt kwenye mchezo pekee wa Bundesliga uliochezwa Ijumaa usiku.

    Aubameyang amefunga bao hilo ambalo ni la 23 msimu huu katika dakika ya 14 ya kipindi cha kwanza akiunganisha krosi safi kutoka kwa nahodha,Marcel Schmelzer aliyekuwa amegongeana vyema na Mjapan Shinji Kagawa aliyekuwa anasherekea miaka 28 ya kuzaliwa.


    Bao hilo siyo kwamba limemfanya Aubameyang aendelee kuwa kinara wa mabao Bundesliga bali pia limeifanya Borussia Dortmund ifikishe pointi 46 baada ya kucheza michezo 25.Pointi tatu nyuma ya RB Leipzig wanaoshikilia nafasi ya pili na pointi 13 nyuma ya vinara Bayern Munich wenye pointi 59.

                                           


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Aubameyang afikisha mabao 23 Bundesliga, Dortmund ikiinyuka Ingolstadt (+ Video) Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top