728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, March 16, 2017

    Mbappe aitwa kwa mara ya kwanza kikosi cha Ufaransa,Lacazette,Benzema,Martial nje


    Kylian Mbappe

    Paris,Ufaransa.

    KOCHA wa timu ya taifa ya Ufaransa,Didier Deschamps,leo mchana ametangaza kikosi cha wachezaji 23 ambacho baadae mwezi huu kitaipeperusha bendera ya nchi hiyo kwenye michezo miwili ya kimataifa.

    Michezo hiyo ni ule wa kuwania tiketi ya kufuzu kombe la dunia dhidi ya Luxembourg na mchezo mwingine utakuwa wa kirafiki dhidi ya Hispania.Michezo yote itapigwa kwenye dimba la Stade de France lililoko Paris.

    Katika kikosi hicho Deschamps amemwita kwa mara ya kwanza kinda mahiri wa AS Monaco ,Kylian Mbappe huku akiendelea kuwafungua vioo nyota kama Karim Benzema wa Real Madrid na Alexandre Lacazette wa Lyon.

    Akiweka wazi sababu za kumwacha Lacazette ambaye yuko kwenye kiwango bora cha upachikaji mabao kwasasa,Deschamps,amesema ameamua kumwita Mbappe ili aweze kumwona kwa ukaribu japo amekiri uwamuzi wa kumwacha Lacazette,25, umekuwa mgumu kwake.

    Wengine walioachwa kwenye kikosi hicho ni pamoja na mshambuliaji mahiri wa Celtic ya Scotland,Moussa Dembele,Antony Martial wa Manchester United Golikipa wa Crystal Palace,Steve Mandanda anayesumbuliwa na goti.

    Kikosi Kamili

    Makipa: Alphonse Areola (Paris St Germain), Benoit Costil (Rennes), Hugo
    Lloris (Tottenham)

    Mabeki: Presnel Kimpembe (PSG),Laurent Koscielny (Arsenal), Layin Kurzawa (PSG), Benjamin Mendy (Monaco), Adil Rami (Sevilla), Bacary Sagna (Manchester City), Djibril Sidibe (Monaco), Samuel Umtiti (Barcelona)

    Viungo: N’Golo Kante (Chelsea),Thomas Lemar (Monaco), Blaise Matuidi (PSG), Paul Pogba (Manchester United),Adrien Rabiot (PSG), Corentin Tolisso (Lyon)

    Washambuliaji: Ousmane Dembele (Borussia Dortmund), Kevin Gameiro (Atletico Madrid), Olivier Giroud (Arsenal), Antoine Griezmann (Atletico Madrid), Kylian Mbappe (Monaco), Dimitri Payet
    (Marseille), Florian Thauvin (Marseille)



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Mbappe aitwa kwa mara ya kwanza kikosi cha Ufaransa,Lacazette,Benzema,Martial nje Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top