728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, March 18, 2017

    Manchester City yapiga bao takatifu England


    Manchester,England.

    Manchester City imepiga bao takatifu England hii ni baada ya kuweka rekodi ya kuwa klabu ya kwanza inayoshiriki ligi kuu nchini humo kuingia mkataba wa kuweka nembo na jina la mdhamini kwenye mikono ya jezi zake.

    Jana Ijumaa usiku Manchester City ilitangaza kuingia mkataba wa kuitangaza kampuni ya kutengeneza matari ya nchini Korea Kusini ya Nexen Tire kupitia mikono ya jezi zake.

    Hatua hiyo ya Manchester City imekuja baada ya hivi karibuni chama cha soka England (FA) kuviruhusu vilabu vya ligi kuu kuwatangaza wadhamini wao wengine kupitia mikono ya jezi zao badala ya kumtangaza mdhamini mmoja pekee tena kifuani peke yake.Lengo kuu ni kuongeza kipato.

    Nexen Tire imekuwa msambazaji rasmi wa matairi ya vyombo vya usafiri vya Manchester City tangu Agosti 2015.Hii itakuwa ni mara yao ya kwanza kwa jina lao kuweka makazi kwenye jezi za Manchester City.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Manchester City yapiga bao takatifu England Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top