728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, March 18, 2017

    Mabingwa Mamelodi waungana na Zesco FC kufuzu makundi ligi ya mabingwa Afrika


    Kampala, Uganda.

    MABINGWA watetezi,Mamelodi Sundowns wameungana na Zanaco FC ya Zambia kutinga hatua ya makundi ya michuano ya klabu bingwa Afrika baada ya jioni hii kutoka sare ya kufungana bao 1-1 na KCCA ya Uganda kwenye mchezo mkali wa marudiano wa hatua ya mtoano uliochezwa hukoPhilip Omondi Stadium,Nambore,Uganda.

    Bao lililowapeleka Mamelodi Sundowns kwenye hatua ya makundi limefunga na mshambuliaji wake Mliberia,Antony Laffor katika dakika ya 80.Kabla ya bao hilo KCCA walikuwa mbele kwa bao moja lililofungwa mapema katika dakika ya 30 ya kipindi cha kwanza na Geoffrey Serunkuma akiunganisha krosi safi ya Brian Majwega.

    Kwa sare hiyo sasa ina maana kwamba Mamelodi Sundowns imefuzu hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2 baada ya kushinda mabao 2-1 katika mchezo wa awali uliochezwa Jumamosi iliyopita kwenye uwanja wa Moses Moripe huko Pretoria, Afrika Kusini.

    Katika mchezo mwingine,Zanaco FC ikiwa nyumbani Lusaka imefuzu hatua ya makundi baada ya kutoka sare ya bila kufungana.Katika mchezo wa awali uliochezwa Dar Es Salaam timu hizo zilitoka sare ya kufungana bao 1-1.

    Vikosi

    KCCA : Ocan, Okot, Kavuma, Awany, Ochaya,Mutyaba, Kirabira, Mucureezi, Okello,Majwega, Serukuuma

    Sundowns: Sandilands, Ngcongca (Laffor 46′),Nascimento, Arendse, Langerman, Kekana,Mabunda (Mashaba 71′), Morena, Zwane,Zakri, Tau

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Mabingwa Mamelodi waungana na Zesco FC kufuzu makundi ligi ya mabingwa Afrika Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top