728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, March 18, 2017

    Chelsea yaizima Stoke City na kuukaribia ubingwa, Leceister City yaikalisha Westham


    Stoke,England.

    CHELSEA imeendelea kuukaribia zaidi ubingwa wa ligi kuu England baada ya jioni hii ikiwa ugenini Bet365 Stadium kuwalaza wenyeji wao Stoke City kwa mabao 2-1. 

    Ikicheza bila ya staa wake,Eden Hazard,Chelsea iliandika bao lake la kwanza katika dakika ya 13 kupitia kwa Willian aliyefunga kwa mkwaju wa adhabu kabla ya mlinzi,Gary Cahill kufunga bao la pili katika dakika ya 87.Bao la Stoke City limefunga na Jon Walters kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 38.

    Matokeo Mengine:Leceister City ikiwa ugenini imeifunga Westham United mabao 3-2.Shukrani kwa mabao ya Riyad Mahrez,Robert Huth na Jamie Vardy.Mabao ya Westham United yamefungwa na Michael Lanzini pamoja na Andrew Ayew.

    Everton ikiwa nyumbani Goodison Park imeifunga Hull City mabao 4-0.Romelu Lukaku amefunga mabao mawili.Sunderland umelazimishwa sare ya 0-0 na Burnley.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Chelsea yaizima Stoke City na kuukaribia ubingwa, Leceister City yaikalisha Westham Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top