Na Mwandishi Wetu
Dar Es Salaam,Tanzania.
KIINGILIO cha chini katika mchezo wa kwanza hatua ya 32 Bora ligi ya Mabingwa Afrika kati ya wenyeji, Yanga SC na Zanaco ya Zambia Jumamosi wiki hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kitakuwa Sh. 3,000.
Akiongea na waandishi wa habari mchana wa leo,Katibu Mkuu wa Yanga,Charles Boniface Mkwasa amesema wameamua kupanga viingilio nafuu ili kutoa fursa kwa mashabiki wa soka nchini kuushuhudia mchezo huo.
Mkwasa amevitaja viingilio vingine vya mchezo huo unaotarajiwa kuwa utakuwa wa vuta nikuvute kuwa ni:VIP A itakuwa Sh.20,000 na VIP B na C itakuwa Sh.15,000.
Habari nyingine njema kuelekea mchezo huo ni kwamba Azam TV imepewa haki ya kurusha moja kwa moja dakika zote tisini za mtanange huo utakaochezeshwa na mwamuzi Aden Abdi kutoka Djibouti.
0 comments:
Post a Comment