Liverpool,England.
Jurgen Klopp amesema kwamba Manchester City ndio timu ngumu kucheza dhidi yao akiwa anakiandaa kikosi chake kukabiliana na vijana wa Guardiola Leo jumapili.
Liverpool wanashika nafasi ya nne kwenye msimamo, pointi moja na nafasi moja nyuma dhidi ya Man City na wameweza kujikusanyia pointi 19 katika michezo 9 dhidi ya vilabu 6 vya juu vya EPL.
"Sidhani kama mechi ya kesho sisi tunapewa kipaumbele, Hiyo sio mbaya sana.Tunajua kwamba sisi huwa tunakuwa wagumu sana kwenye mechi kama hizi. Hiyo ni ukweli."
"Tumekuwa kwenye hali nzuri sana kwenye mechi kama hizi mpaka sasa lakini kwangu mimi Man City ndio klabu ngumu sana kucheza dhidi yao Ni soka kweli kweli na ngumu sana kuzuia."
"Lazima tuwe kwenye ubora wetu ili kupata chochote kwenye mechi yenyewe. Kama ukizubaa kidogo watakusumbua sana na uwezo wao wa kupiga pasi . Naisubiria kwa hamu sana. Ni mechi ya changamoto ya kimbinu."
0 comments:
Post a Comment