Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amethibitisha leo kwamba tayari ameshafanya maamuzi kuhusu mustakabali wake ndani ya klabu ya Arsenal na atautangaza huo uamuzi siku za hivi karibuni.
Baada ya klabu yake kupoteza mechi 4 kati ya 5 zilizopita dhidi ya West Brom leo na kuwaacha pointi 6 kutoka nafasi nne za juu zikiwa zimebaki mechi 11 msimu kuisha , wenger amesema kikosi chake kipo kwenye hali mbaya.
"Usijali, najua nini nitafanya katika maisha yangu ya baadae na siku za hivi karibuni mtajua, tena siku si nyingi sana." Alisema Wenger akiwa na waandishi wa Habari baada ya mechi.
"Mtaona. Leo siwezi kuhofia kuhusu mustakabali wangu.Tupo kwenye kipindi cha kipekee sana ambacho hatujawahi kuwa kwa kipindi cha miaka 20. Sasa hivi tunapoteza mechi hadi mechi , na hiyo ndio muhimu kwangu kufikiria kuliko mustakabali wangu."
0 comments:
Post a Comment