728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, March 19, 2017

    Zidane tulimtaka Mbappe



    Madrid,Hispania.

    Zinedine Zidane amethibitisha kwamba Real Madrid ilikaribia kumnasa kinda Kylian Mbappe kabla hajajiunga na Monaco.

    Real Madrid wamekuwa wakimuhusudu kwa muda mrefu sana kinda huyo wa kimataifa wa Ufaransa ambaye kwasasa anawindwa na vilabu vingi sana barani Ulaya.

    Mbappe alijiunga na kikosi cha vijana cha Monaco mwaka 2013 lakini Zidane ameweka wazi kwamba alikuwa na nafasi ya kujiunga na Real Madrid.

    "Alikuwa anakaribia kusaini Real Madrid lakini akaenda Monaco."

    "Ni mchezaji mzuri sana. Anachokifanya katika umri wake ni cha ajabu sana , lakini kitu muhimu kwangu ni kufikiria tutakachokifanya kwenye mechi ya leo ( Dhidi ya Athletico Bilbao)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Zidane tulimtaka Mbappe Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top