Manchester City wanajiandaa kutoa kitita cha pauni milioni 30 kwa ajili ya beki wa AS Roma, Antonio Rudiger, kwa mujibu wa taarifa kutoka Daily Mirror.
Beki huyo wa kimataifa wa Ujerumani ametajwa kuwa chaguo la kwanza la Guardiola ambaye yupo kwenye harakati za kusuka upya safu yake ya ulinzi inayoruhusu sana magoli.
Mirror limearifu kwamba maskauti wa Man City wamekuwa wakimfuatilia mara kwa mara Rudiger katika wiki za hivi karibuni na huenda wakakutana na wawakilishi wa Rudiger mapema wiki ijayo.
Chelsea nao walikuwa wakihusishwa na beki huyo majira ya kiangazi yaliyopita na City wameonesha shauku ya kutengeneza pacha pamoja na John Stones katika moyo wa safu yao ya ulinzi.
0 comments:
Post a Comment