728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, March 19, 2017

    Manchester City vs Liverpool ; Ni vita ya Guardiola vs Klopp


    Manchester,England.

    Baada ya kushinda mechi mbili mfululizo za Ligi kwa mara ya kwanza mwaka huu, Liverpool watakuwa wageni Etihad kumenyana na Manchester City katika mchezo wa Ligi Kuu Uingereza.


    Liverpool watakutana na Manchester City iliyojeruhiwa na Monaco kwa kuchapwa mabao 3-1 na kutupwa nje ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.


    Unapozungungumzia mbio za ‘top four’ basi hili ni moja ya pambano kubwa linaloweza kumbeba mshindi katika mbio hizo tamu.

    Kwa mara ya mwisho, timu hizo zilikutana kwenye mkesha wa kuukaribisha mwaka 2017 kwenye uwanja wa Anfield, ambapo Liverpool waliibuka na ushindi wa bao 1-0.Katika mechi sita za mwisho walizokutana, Liverpool wameshinda 5 huku wakitamba zaidi kwa kushinda mechi 4 mfululizo.

    Guardiola v Klopp

    Hii itakuwa mara ya kumi kwa Guardiola na Klopp kupambana huku Mjerumani wa Liverpool akimtambia Mhispaniola kwa kutoa vipigo mara tano.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Manchester City vs Liverpool ; Ni vita ya Guardiola vs Klopp Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top