Bandung,Indonesia.
BAADA ya kuwa kijiweni kwa muda mrefu akiwa hana timu ya kuchezea, hatimaye leo jioni kiungo wa zamani wa Chelsea na Ghana,Michael Essien amejiunga na timu ya Persib Bandung ya nchini Indonesia.
Essien,34,amejiunga na Persib Bandung kwa mkataba wa mwaka mmoja na atakuwa akilipwa mshahara wa Euro laki nane (800,000) kwa mwaka na kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi katika historia ya soka la nchini ya Indonesia.Pia atakuwa akivalia jezi yake kipenzi,namba 5.
Mwenyekiti wa Persib Bandung,Teddy Tjahyono amesema timu yake imeamua kumsajili Essien aliyewahi pia kuzichezea timu za Real Madrid AC Milan ili kupandisha thamani ya ligi ya Indonesia.
Essien anakuwa mchezaji wa tatu kujiunga na timu za Indonesia baada ya gwiji wa zamani wa Cameroon, Roger Milla na mshindi wa kombe la dunia Muargentina,Mario Kempes aliyecheza Indonesia katika miaka ya 1990.
0 comments:
Post a Comment