728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, March 14, 2017

    Neymar awashiwa taa za kijani kuivunja rekodi ya Pele Brazil

    Rio de Janeiro,Brazil.

    NAHODHA wa zamani wa Brazil,Cafu anaamini staa wa sasa wa nchi hiyo,Neymar ana nafasi kubwa ya kumpiku gwiji wa zamani wa nchi hiyo Pele na kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Brazil.

    Pele mshindi mara tatu wa kombe la dunia kwasasa ndiye mfungaji bora wa muda wote wa Brazil akiwa amefunga mabao 77 katika michezo 91sawa na wastani wa bao 0.84 kwa kila mchezo mmoja.

    Neymar mwenye umri wa miaka 25 sasa anashikilia nafasi ya nne kwenye chati za upachikaji nchini Brazil akiwa tayari amefunga mabao 50 katika michezo 75 sawa na wastani wa mabao 0.66 kwa kila mchezo mmoja.

    Takwimu hizo zimemfanya Cafu,46, mshindi mara mbili wa kombe la dunia aamini kuwa Neymar ana kipaji na muda wa kuweza kumpiku Pele ambaye anasemekana kuwa ndiye msukuma kandanda bora zaidi kuwahi kutokea duniani.

    "Neymar bado ni mdogo na ana muda mwingi mbele yake.Kama ataendelea kucheza kama anavyocheza sasa basi kuna kila uwezekano kuwa atampiku Pele.Amesema Cafu anayeshikilia rekodi ya kuichezea Brazil michezo mingi zaidi kuliko wachezaji wote wa nchi hiyo.Jumla ameichezea michezo 142.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Neymar awashiwa taa za kijani kuivunja rekodi ya Pele Brazil Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top